<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi atoa?salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Baraza la Rais wa Libya huku idadi ya vifo vinavyotokana na mafuriko ikivuka 3,000

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 13, 2023
    Rais Xi atoa?salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Baraza la Rais wa Libya huku idadi ya vifo vinavyotokana na mafuriko ikivuka 3,000
    Picha iliyopigwa Septemba 11, 2023, ikionyesha eneo lililoathiriwa na mafuriko huko Derna, Libya. (Serikali yenye makao yake mashariki mwa Libya/ Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kwa Mohamed Menfi, Mwenyekiti wa Baraza la Rais wa Libya, kutokana na kutokea kwa dhoruba iliyoambatana na mvua kubwa na kuleta mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu wengi nchini Libya.

    Kwenye ujumbe wake huo alioutuma siku ya Jumanne, Rais Xi amesema baada ya kufahamishwa kuhusu dhoruba hiyo iliyosababisha vifo na majeruhi kwa watu wengi na hasara ya mali nchini Libya, anaomboleza watu wanaofariki katika maafa hayo na kutoa salaumu za rambirambi za dhati kwa familia zilizofiwa na watu waliojeruhiwa kwa niaba ya serikali na watu wa China.

    Rais Xi ameelezea imani yake kwamba watu wa Libya bila shaka watashinda matatizo pamoja na maafa.

    Wakati huohuo, idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko hayo makubwa yaliyokumba mji wa mashariki mwa Libya wa Derna siku ya Jumapili imeongezeka hadi kufikia 3,060, huku wengine 5,200 wakiwa bado hawajulikani waliko, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani yenye makao yake Mashariki mwa Libya iliyotolewa siku hiyo ya Jumanne.

    "Mamlaka zimezika miili ya watu 2,800 baada ya familia zao kuwatambua, huku miili ya watu 260 ambayo haijatambuliwa bado iko katika hospitali ya mji huo," msemaji wa wizara hiyo Tareq al-Kharraz ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

    Al-Kharraz amesema watu 5,200 bado hawajulikani walipo, akisisitiza kwamba idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi, ikizingatiwa kuwa kazi za utafutaji na uokoaji zinaendelea, na miili zaidi ya watu inaendelea kupatikana kutoka maeneo mbalimbali ndani ya mji.

    Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, utoaji msaada na uokoaji umeanza kufika Derna siku ya Jumanne, ikiwa ni zaidi ya saa 36 kupita tangu maafa kukumba mji huo wa pwani. Mafuriko hayo yalikuwa yameharibu sana au kubomoa kabisa barabara nyingi za kuingia katika mji huo, ambao ni makazi ya takriban wakaazi 89,000.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha