<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake Maduro wa Venezuela watangaza kuinua uhusiano kati ya China na Venezuela (2)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2023
    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake Maduro wa Venezuela watangaza kuinua uhusiano kati ya China na Venezuela
    Rais Xi Jinping wa China akikutana na mwenzake wa Venezuela Nicolas Maduro Moros, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 13, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na mwenzake wa Venezuela, Nicolas Maduro Moros kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing siku ya Jumatano. Marais hao wawili wametangaza kuinua uhusiano kati ya China na Venezuela kuwa wenzi wa kimkakati wa siku zote.

    Ushirikiano wa kimkakati wa siku zote

    Rais Xi amesema China na Venezuela ni marafiki wazuri wanaoaminiana na washirika wazuri katika kutafuta maendeleo kwa pamoja, akipongeza urafiki wa chuma ulioanzishwa katikati ya mabadiliko ya kila mara ya mazingira ya kimataifa.

    "China daima imekuwa ikitazama uhusiano wake na Venezuela kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na inaunga mkono kwa dhati juhudi za Venezuela za kulinda mamlaka ya nchi, heshima ya taifa, na utulivu wa jamii, pamoja na mapambano ya haki ya Venezuela dhidi ya uingiliaji kati wa nje," Rais Xi amemwambia Rais Maduro.

    Amesema, kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa siku zote kati ya China na Venezuela kunakidhi matarajio ya pamoja ya watu wa pande hizo mbili na kuendana na mwelekeo wa jumla wa maendeleo ya kihistoria.

    Kwa upande wake Rais Maduro amesema Venezuela na China zinafurahia urafiki wa pande zote na ushirikiano wenye manufaa, na kufanya uhusiano wa nchi hizo mbili kuwa mfano wa uhusiano kati ya nchi za Duni ya Kusini.

    Haiba ya China

    Rais Xi amezungumzia mageuzi na ufunguaji mlango wa China, hasa maendeleo ya maeneo maalum ya kiuchumi, na kusisitiza kuwa mageuzi na ufunguaji mlango ni nyenzo muhimu kwa China ili kuendana na nyakati kwa hatua kubwa na ni uamuzi muhimu katika kuifanya China kuwa ilivyo leo.

    "China inathamini uzoefu wa thamani uliopatikana katika mchakato huu na itaendelea kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango. Hakuna nguvu inayoweza kuzuia maendeleo na hatua za kimaendeleo za China," Rais Xi amesema.

    Kwa upande wake Rais wa Venezuela amesema kuwa, nchi yake inaunga mkono Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, amesema China imekuwa nchi kubwa iliyojitolea kwa amani, maendeleo, na ustawi wa binadamu, na pia ni injini muhimu ya kuhimiza kuleta dunia mpya yenye ncha nyingi.

    Kupanua ushirikiano

    Rais Xi amesema, China iko tayari kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa China na Venezuela, na pande hizo mbili zinapaswa kufanya kazi kwa karibu katika mifumo ya ushirikiano wa pande nyingi, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Kundi la 77 (G77) na China, kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi nyingine zinazoendelea, kulinda kwa pamoja madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha