<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atoa wito kwa Mkoa wa Zhejiang kuandika ukurasa mpya wa Zhejiang katika kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China (4)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2023
    Rais Xi Jinping atoa wito kwa Mkoa wa Zhejiang kuandika ukurasa mpya wa Zhejiang katika kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China
    Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitembelea soko la biashara ya kimataifa wakati akikagua Mji wa Yiwu wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 20, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    HANGZHOU, Zhejiang/ZAOZHUANG, Shandong, - Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameutaka Mkoa wa Zhejiang, Mashariki wa China kufanya jitihada kubwa kuandika ukurasa mpya wa Zhejiang katika kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China.

    Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mkoa huo kuanzia Septemba 20 hadi 21, Rais Xi ametoa wito kwa mkoa huo kutillia maanani kujenga eneo la vielelezo vya ustawi wa pamoja wa watu, na kujijenga kuwa dirisha muhimu la kuonyesha nguvu za ujamaa wenye umaalum wa China katika zama mpya.

    Katika ziara yake, Rais Xi ametembelea miji ya Jinhua na Shaoxing, ambako alikagua maeneo ya vijiji, soko la biashara, ukumbi wa maonyesho na bustani ya utamaduni.

    Akiwa njiani kurejea Beijing, Rais Xi pia ametembelea Mji wa Zaozhuang wa Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China.

    Asubuhi ya Septemba 20, Rais Xi alikagua Kijiji cha Lizu huko Jinhua. Akiwa kijiji hapo, alifurahi kufahamishwa kwamba mapato ya kila mwaka ya kila mtu katika kijiji hicho yalikuwa yamefikia yuan 52,000 (kama dola 7,250 za Kimarekani)

    “Kijiji cha Lizu kimepata maendeleo dhahiri katika kuhimiza ustawi wa pamoja wa watu wote”, Rais Xi amesema, akielezea matumaini kwamba kijiji hicho kitafanya juhudi zaidi na kupata matokeo zaidi katika kuendeleza ustawishaji vijijini.

    Baadaye, Rais Xi alitembelea Soko la Biashara ya Kimataifa la Yiwu mjini Jinhua, ambako alifahamishwa kuhusu uendeshaji wa soko hilo na treni za mizigo za China na Ulaya. Rais Xi amehimiza soko hilo la biashara kuchangia zaidi katika kupanua masoko ya ndani na nje ya nchi na pia kurahisisha mzunguko wa uchumi wa China na wa kimataifa.

    Septemba 21, Rais Xi alitembelea serikali ya Mkoa wa Zhejiang. Amekiri mafanikio ambayo Zhejiang imepata katika sekta mbalimbali na kutoa maagizo zaidi kwa mkoa huo.

    Rais Xi ameuagiza Mkoa wa Zhejiang kutangulia mbele katika kujenga nguvu mpya za maendeleo kupitia uvumbuzi wa kisayansi, kuendeleza uchumi halisi kuwa msingi wa kujenga mfumo wa kisasa wa viwanda, kutekeleza jukumu kuu na kuwa mfano katika kuhimiza zaidi ustawi wa pamoja wa watu wote, kupunguza pengo kati ya miji na vijiji; pamoja na kushughulikia tofauti za maendeleo na mapato kati ya maeneo na sehemu za mkoa huo.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha