<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Wanasayansi wa Kenya na China wazindua chapisho la kwanza la kitaifa la kuhifadhi kumbukumbu za mimea ya Kenya (3)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2023
    Wanasayansi wa Kenya na China wazindua chapisho la kwanza la kitaifa la kuhifadhi kumbukumbu za mimea ya Kenya
    Watu wakihudhuria hafla ya kutolewa kwa kitabu cha juzuu ya 23 "Rubiaceae" ya kitabu cha Mimea ya Kenya huko Nairobi, Kenya, Septemba 25, 2023. (Xinhua/Li Yahui)

    NAIROBI - Wanasayansi kutoka China na Kenya wamezindua juzuu ya 23 ya Kitabu cha Mimea (Flora) ya Kenya huko Nairobi, Kenya, kuashiria chapisho la kwanza la kitaifa kuhusu mimea ya Kenya na kujaza pengo la machapisho lililokuwepo katika nyanja ya utafiti wa rasilimali za mimea nchini humo.

    Kitabu cha Flora ya Kenya, ambacho kimegawanywa katika juzuu 31, kitaweka kumbukumbu za aina za mimea karibu 7,000 kutoka familia 223 za nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Juzuu ya 23 "Rubiaceae," ya kitabu hicho ni sehemu ya kwanza ya mradi huo iliyochapishwa rasmi Jumatatu na Shirika la Uchapishaji wa Machapisho ya Sayansi na Teknolojia la Hubei na Shirika la Historia ya Mazingira ya Asili la Afrika Mashariki.

    Ni mradi wa utafiti wa ushirikiano unaohusisha wanasayansi kutoka Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (CAS), Kituo cha Pamoja cha Utafiti cha China na Afrika (SAJOREC) na Makavazi ya Taifa ya Kenya.

    Mary Gikungu, Mkurugenzi Mkuu wa Makavazi ya Taifa ya Kenya, amesema kutolewa kwa chapisho hilo linaloelezea utajiri wa mimea nchini Kenya kutatoa habari zaidi kuhusu juhudi za kuihifadhi na kuchochea ukuaji wa kijani. "Kitabu ambacho tumekizindua hivi punde ni muhimu sana kwa sababu kinatoa utambulisho wa mimea ya Kenya."

    Amepongeza ushirikiano kati ya wanasayansi wa China na Kenya, akisema kuwa umeingiza uhai katika uhifadhi wa spishi ambazo ni muhimu kwa usalama wa chakula na ustahimilivu wa tabianchi nchini humo. Kupitia ushirikiano na China, Makavazi ya Taifa ya Kenya yameweza kuwajengea uwezo watafiti wake ili kuendeleza uhifadhi wa makazi ya viumbe katika ngazi ya chini, Gikungu amesisitiza.

    Liu Weidong, Mkurugenzi wa Ofisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya CAS, amesema kuwa Kitabu cha Flora ya Kenya kitaangazia hifadhi kubwa ya spishi za mimea nchini humo na kufahamisha uhifadhi wake endelevu.

    Watu wanashiriki kwenye hafla ya kutolewa kwa juzuu ya 23 "Rubiaceae" ya kitabu cha Mimea ya Kenya mjini Nairobi, Kenya, Septemba 25, 2023. (Xinhua/Li Yahui)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha