<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atoa heshima kwa mashujaa wa Kitaifa katika Siku ya Mashujaa Waliojitoa Mhanga kwa Taifa la China (4)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 02, 2023
    Rais Xi Jinping atoa heshima kwa mashujaa wa Kitaifa katika Siku ya Mashujaa Waliojitoa Mhanga kwa Taifa la China
    Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali ya China wakitembea kuzunguka Mnara wa Mashujaa wa Umma kutoa heshima zao kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing, China, Septemba 30, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

    BEIJING – Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali ya China ikiwa ni pamoja na Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wamehudhuria hafla ya Jumamosi asubuhi hapa Beijing ya kuwasilisha vikapu vya maua kwa mashujaa wa Taifa la China walioaga Dunia.

    Hafla hiyo imefanyika kuadhimisha Siku ya 10 ya Mashujaa wa China waliojitoa Mhanga, siku moja kabla ya Siku ya Taifa la China, ambayo imeadhimisha jana Jumapili, Oktoba 1.

    Saa 4 Asubuhi (saa za Beijing), washiriki wote waliimba wimbo wa taifa wa China, na kisha kutoa heshima za kukaa kimya kwa muda kwa ajili ya mashujaa waliojitoa mhanga na kupoteza maisha yao kwa ajili ya ukombozi wa watu wa China na maendeleo ya Jamhuri ya Watu wa China.

    Vikapu tisa vikubwa vya maua viliwekwa mbele ya Mnara wa Mashujaa wa Umma. Rais Xi na viongozi wengine walitembea hadi chini ya mnara huo, ambapo alinyoosha utepe kwenye vikapu kabla ya kuwaongoza maafisa wengine waandamizi katika matembezi kuzunguka mnara huo kutoa heshima zao.

    Vikapu hivyo, vikiwa na tepe zenye maandishi yanayosomeka "Utukufu wa Milele kwa Mashujaa wa Umma," ziliwasilishwa kwa jina la Kamati Kuu ya CPC; Bunge la Umma la China; Baraza la Serikali la China; Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China; Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC); vyama vingine vya siasa vya China, Shirikisho la Viwanda na Biashara la China na wazalendo wasio na misimamo ya vyama; mashirikisho ya umma na watu kutoka nyanja zote za maisha; maveterani, makada waandamizi waliostaafu na jamaa za mashujaa waliojitolea mhanga; na kikosi cha Watoto Watangulizi.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha