<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mkutano Mkuu wa 18 wa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China (ACFTU) wafunguliwa (3)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2023
    Mkutano Mkuu wa 18 wa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China (ACFTU) wafunguliwa
    Mkutano wa 18 wa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la vya China (ACFTU) ukifunguliwa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la mjini Beijing, China, Oktoba 9, 2023. (Xinhua/Cai Yang)

    Beijing - Mkutano wa 18 wa wajumbe wa nchi nzima wa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China (ACFTU) umefunguliwa siku ya Jumatatu asubuhi mjini Beijing.

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) alihudhuria ufunguzi wa mkutano huo pamoja na viongozi wengine waandamizi wa CPC na serikali.

    Mjumbe wa Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, Cai Qi akiwa kwa niaba ya kamati kuu ya Chama ametoa pongezi za dhati kwa mkutano huo na kutoa salamu za dhati kwa wafanyakazi na maofisa wa mashirikisho ya wafanyakazi kote nchini China.

    Cai amesema, “Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha CPC Mwaka 2012, wafanyakazi wa China wameshikamana kwa karibu na Kamati Kuu ya CPC, wamebeba majukumu mazito kwa ujasiri, wamefanya kazi kwa bidii na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuhimiza mambo ya Chama na nchi kupata mafanikio ya kihistoria na kufanya mageuzi ya kihistoria.

    Amesema, katika miaka mitano iliyopita, kwa kushikilia mwongozo wa Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya, na kuimarisha ujenzi wa chama, kuendeleza mageuzi na uvumbuzi, na kuimarisha fikra na siasa ya wafanyakazi, mashirikisho ya wafanyakazi yamehimiza mageuzi ya ujenzi wa wafanyakazi wa viwanda, kutekeleza majukumu yao katika kulinda haki za wafanyakazi, kuhimiza uhusiano wa kikazi wenye maafikiano, na kuhamasisha wafanyakazi kufanya juhudi za kutoa mchango mpya katika zama mpya, na kuanza safari mpya pamoja na watu wa nchi nzima katika kujenga nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha