<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping akagua kazi ya urejeshaji na ukarabati baada ya maafa ya Beijing na Hebei (2)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2023
    Rais Xi Jinping akagua kazi ya urejeshaji na ukarabati baada ya maafa ya Beijing na Hebei
    Asubuhi ya tarehe 10, Novemba, Rais Xi Jinping wa China aliwasiliana na walimu na wanafunzi katika Shule ya Makabila ya Mlima Miaofeng ya eneo la Mentougou la Beijing. (Picha ilipigwa na Sheng Jiapeng/Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) tarehe 10 alikagua kazi ya kurejesha hali na kujenga upya baada ya maafa mjini Beijing na mkoa wa Hebei wa China, ambapo alisisitiza kuwa, kamati ya chama na serikali kwenye ngazi zote, pamoja na pande nyingine husika zinatakiwa kutekeleza kwa makini mpango wa kamati kuu ya chama, kufanya juhudi zaidi za kuongoza vizuri kazi ya kurejesha hali na kujenga upya baada ya maafa, na kuhakikisha watu wanafanya kazi na kuishi maisha kwa utulivu na kushinda majira ya baridi katika nyumba zenye hali joto. Ni lazima kushikilia kuweka umma kwenye kiini cha kazi, kushikilia mtazamo wa kimfumo, kufuata ukweli wa mambo na hali halisi, kufanya mpangilio kwa njia ya kisayansi na kwa kufaa, kuondoa pengo na upungufu kwa kasi, na kuharakisha kukamilisha mfumo wa kuzuia mafuriko ya maji na mfumo wa usimamizi wa hali ya dharura, ili kuongeza hatua kwa hatua uwezo wa kuzuia maafa, kupunguza hasara na kufanya uokoaji wakati wa maafa.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha