Lugha Nyingine
Habari Picha: Mazingira ya asili ya sehemu ya Jumba la Makumbusho la Bustani ya Kitaifa ya Jiolojia ya Peninsula ya Dapeng ya Shenzhen, China
Picha hii iliyopigwa Novemba 16, 2023 ikionyesha mwonekano wa mbele wa Jumba la Makumbusho la Bustani ya Kitaifa ya Jiolojia ya Peninsula ya Dapeng ya Shenzhen, China. (People’s Daily Online) |
Jumba la Makumbusho la Bustani ya Jiolojia ya Kitaifa ya Peninsula ya Dapeng liko katika sehemu ya vivutio vya utalii ya Qiongqiu ya Bustani ya Kitaifa ya Jiolojia ya Shenzhen, China. Ni moja ya vivutio vikuu vya bustani hiyo. Jumba hilo ni lenye usanifu rahisi na la kifahari, likiwa na mwonekano wa kama miamba ya volkeno iliyotawanyika chini ya Mlima Qiniang, likichanganyika katika mazingira ya asili yanayolizunguka. Lina jumla ya kumbi sita za maonyesho: Ukumbi wa Utangulizi, Ukumbi wa Kuielewa Dunia, Ukumbi wa Peninsula ya Dapeng, Ukumbi wa Madini, Ukumbi wa Mazingira ya Mijini na Kijiolojia, na Jumba la Maonyesho ya Muda Mfupi. Ni mahali pazuri pa kuunganisha utafiti wa kisayansi, uenezaji wa sayansi, kutazama mandhari ya mazingira ya asili, kufanya mapumziko, burudani na kufurahia mawe yenye maumbo ya ajabu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma