Lugha Nyingine
Xi Jinping akutana na Ma Ying-jeou na ujumbe wa vijana wa Taiwan mjini Beijing
BEIJING - Xi Jinping, ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amekutana na Ma Ying-jeou na ujumbe wa vijana wa Taiwan mjini Beijing siku ya Jumatano, ambapo amesema watu wa pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan wote ni Wachina na kwamba "Hakuna mafundo ambayo hayawezi kufunguliwa, hakuna masuala ambayo hayawezi kujadiliwa, na hakuna nguvu inayoweza kututenganisha".
Rais Xi amesema, ndugu wa pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan ni wa Taifa moja la China, historia ya zaidi ya miaka 5,000 ya Taifa la China ilishuhudia vizazi vilivyofuatana vya mababu wakihama na kuishi katika eneo la Taiwan na watu kutoka pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan kupigana bega kwa bega ili kuokoa kisiwa hicho kutoka kwa wavamizi wa kigeni.
Umbali wa Mlango wa Bahari hauwezi kutenganisha uhusiano wa kiukoo kati ya ndugu wa pande mbili za Mlango Bahari huo, Rais Xi amesema.
Amesema kuwa tofauti katika mifumo haibadilishi ukweli kwamba pande mbili za Mlango Bahari wa Taiwan ni za China moja, na uingiliaji kati wa nje hauwezi kurudisha nyuma mwelekeo wa kihistoria wa muungano wa Taifa la China.
Rais Xi akisema, vijana ni "matumaini ya nchi na mustakabali wa taifa," amewahimiza vijana wa pande mbili za Mlango Bahari wakiwa Wachina ni lazima kuwa na nia thabiti, matamanio ya kujivunia, kujiamini, na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ustawi wa muda mrefu wa Taifa la China, na kuendelea kujenga utukufu mpya wa taifa hilo.
Ndugu wa pande mbili za Mlango Bahari wanapaswa kupinga kwa uthabiti shughuli zote za makundi yanayotaka “Taiwan ijitenge" na uingiliaji wa nchi za nje, Rais Xi amesema, huku akitoa wito wa kufuata kwa pamoja mustakabali mzuri wa muungano wa taifa wa amani.
Amesisitiza umuhimu mkubwa wa kutilia maanani Makubaliano ya Mwaka 1992, ambayo yanajumuisha kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kuwa na uelewa wa pamoja kwamba pande mbili za Mlango Bahari wa Taiwan ni za nchi moja na taifa moja.
Kwa upande wake Ma Ying-jeuo amesema kwamba kushikilia Makubaliano ya 1992 na kupinga kuifanya " Taiwan ijitenge" ni msingi wa pamoja wa kisiasa kwa maendeleo ya amani ya uhusiano wa pande mbili za Mlango Bahari wa Taiwan.
Watu wa pande mbili za Mlango Bahari ni wa taifa moja la China, na wanapaswa kuzidisha mabadilishano na ushirikiano, kuendeleza kwa pamoja utamaduni wa China, kuboresha ustawi wa ndugu wa pande mbili, na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ustawishaji wa Taifa la China, Ma amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma