<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    China na Ufaransa zajiandaa kuimarisha uhusiano wakati hali ya kimataifa inashuhudia mabadiliko (3)

    (CRI Online) Mei 06, 2024
    China na Ufaransa zajiandaa kuimarisha uhusiano wakati hali ya kimataifa inashuhudia mabadiliko
    Mchana wa Tarehe 5, Mei kwa saa za Paris, Rais Xi Jinping wa China aliwasili Paris kwa ndege maalumu, na kuanza kufanya ziara ya kiserikali nchini Ufaransa kutokana na mwaliko wa Rais Emmanuel Macron. (Picha na Xie Huanchi/Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China jana Jumapili aliwasili Paris kwa ziara ya kiserikali nchini Ufaransa, ambapo nchi hizi mbili zimejiandaa kuimarisha uhusiano kati yao na kusisitiza ahadi yao ya kuongeza ushirikiano wakati hali ya kimataifa inashuhudia mabadiliko.

    Majadiliano na makubaliano kwenye ziara ya tatu ya kiserikali ya Rais Xi nchini Ufaransa, kufuatia ziara zake zilizopita katika mwaka wa 2014 na 2019, yanatarajiwa kuhusisha nyanja nyingi muhimu. Kutoka biashara na uwekezaji hadi uvumbuzi na mawasiliano ya kiutamaduni, ajenda ya ziara hiyo inaakisi uhusiano unaohusisha nyanja zote kati ya China na Ufaransa.

    Katika ziara hiyo, viongozi wa nchi hizo mbili pia wanatarajiwa kubadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa wanayoyafuatilia kwa pamoja, na ushirikiano wa pande nyingi.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha