Lugha Nyingine
Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wafanya mazungumzo (3)
Asubuhi ya tarehe 6, Mei kwa saa za Paris, Rais wa China Xi Jinping alialikwa katika kufanya mazungumzo ya pande tatu kati yake na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen katika Ikulu ya Elysee huko Paris, Ufaransa.
Katika mazungumzo hayo Rais Xi amedhihirisha kuwa, China siku zote inachukulia Ulaya kama mwelekeo muhimu wa mambo ya diplomasia ya China yenye umaalumu wa nchi kubwa, na kuchukulia Ulaya kuwa ni mwenzi muhimu katika kutimiza maendeleo ya mambo ya kisasa yenye umaalumu wa China. Anatumai uhusiano wa China na Ufaransa na uhusiano wa China na Ulaya zinaweza kuhimizana na kupata maendeleo kwa pamoja. Hivi sasa Dunia imeingia katika kipindi kipya cha msukosuko na mabadiliko. China na Ulaya zikiwa nguzo muhimu zinatakiwa kushikilia msimamo wao wa kuwa wenzi na kushikilia kufanya mazungumzo na ushirikiano, ili kusukuma mbele maendeleo mazuri ya uhusiano wa China na Ulaya, na kutoa mchango mpya siku hadi siku kwa ajili ya amani na maendeleo ya Dunia.
Kwa upande wake Rais Macron alisema, anafurahi sana kufanya mazungumzo ya viongozi wa pande hizo tatu wakati Rais Xi anapofanya ziara ya tatu ya kiserikali nchini Ufaransa. Hivi sasa Dunia inakabiliwa na changamoto kubwa, na Ufaransa na Umoja wa Ulaya zinahitaji kuimarisha ushirikiano na China zaidi kuliko wakati wowote katika historia. Upande wa Ulaya haukubali kinachoitwa “Kutenganishwa Kiuchumi”, na unakaribisha kampuni za China kuwekeza katika Ulaya.
Von der Leyen alisema, uhusiano kati ya Ulaya na China ni mzuri, na mwaka ujao utakuwa maadhimisho ya miaka 50 tangu Umoja wa Ulaya na China zilipoanzisha uhusiano wao wa kibalozi. Umoja wa Ulaya ungependa kuheshimiana na China, kutafuta maoni ya pamoja huku kukiweka tofauti pembeni. Upande wa Ulaya unapongeza juhudi za China na mafanikio yaliyopatikana katika kubadilisha muundo wa viwanda ili kupata maendeleo yasiyochafua mazingira, ukitumai kuendelea na mazungumzo na China kwa udhati na unyofu na kuimarisha ushirikiano kati yao.
Kuhusu msukosuko wa Ukraine, Xi alisema, pande za China, Ufaransa na Ulaya zote zina matumaini ya kusimamisha vita haraka iwezekanavyo na kurudisha amani katika Ulaya, na zote zinaunga mkono kutatua msukosuko wa Ukraine kwa njia ya kisiasa. Upande wa China si mzusha wa msukosuko huo wala si mhusika wake, na siku zote China inajitihada kuhimiza mazungumzo ya amani. China ingependa kuendelea na mawasiliano na pande husika.
Kuhusu mgongano kati ya Palestina na Israeli, Xi alisisitiza kuwa, kwa sasa mambo ya dharura zaidi ni kusimamisha vita kwa pande zote , na mambo muhimu zaidi ni kuhakikisha uokoaji wa kibinadamu, na utatuzi wa mwisho ni kutekeleza “Mpango wa Nchi Mbili”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma