<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Marais wa China na Serbia wafanya mazungumzo mjini Belgrade

    (CRI Online) Mei 09, 2024
    Marais wa China na Serbia wafanya mazungumzo mjini Belgrade
    Asubuhi ya tarehe 8, Mei, rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo na rais Aleksandar Vucic huko Belgrade, Serbia. (Picha na Li Xueren/Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic walifanya mazungumzo Jumatano mjini Belgrade.

    Xi alisema urafiki kati ya China na Serbia umestahimili jaribio la misukosuko ya kimataifa na una urithi wa kihistoria, msingi thabiti wa kisiasa na maslahi ya pamoja.

    Xi alisema chini ya uongozi wa Rais Vucic, Serbia imepata maendeleo ya haraka ya kiuchumi na hali ya maisha ya watu wake imeendelea kuboreshwa.

    Xi aliongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Serbia katika kudumisha na kuendeleza urafiki wa pande hizo mbili, kulinda maslahi ya msingi na ya muda mrefu ya nchi hizo mbili na kutafuta maendeleo na ustawi wa taifa, kwa lengo la kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Serbia yenye mustakabali wa Pamoja katika zama mpya.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha