<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Shughuli za ghasia dhidi ya serikali yatikisa Kenya kwa wiki tatu mfululizo (4)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2024
    Shughuli za ghasia dhidi ya serikali yatikisa Kenya kwa wiki tatu mfululizo
    Polisi wa kutuliza ghasia wakipambana na waandamanaji jijini Nairobi, Kenya, Julai 2, 2024. (Picha na Sheikh Maina /Xinhua)

    NAIROBI - Shughuli za ghasia zimezuka katika sehemu mbalimbali nchini Kenya siku ya Jumanne, zikisababisha vifo vya watu wasiopungua wawili, huku waandamanaji wanaoipinga serikali wakiendelea na maandamano yao kwa wiki ya tatu mfululizo ambapo hali ya ghasia imeendelea ingawa Rais William Ruto ameuondoa bungeni muswada unaotakiwa kujadiliwa na kutolewa kuhusu hatua za ushuru Juni 26, ambao awali ndiyo ulizua maandamano hayo.

    Shughuli ya Jumanne ya kupinga serikali iliambatana na kufunga barabara, maduka kuporwa, magari kuteketezwa, kurushiana risasi, uchomaji wa matairi na wizi. Jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, biashara zilifungwa, usafiri ulisimama, na wakaazi walikwepa eneo la katikati ya mji la kibiashara (CBD), ambapo mamia ya vijana walikuwa wakipambana na polisi katika mapigano ya kukimbia.

    "Haya siyo maandamano ya kuipinga serikali niliyokuwa nikitazamia. Nilidhani kila kitu kingekuwa cha amani isipokuwa mapigano ya hapa na pale na polisi, lakini leo kulikuwa na vurugu na wizi kila mahali," amesema Lewis Kimeu, mwandamanaji kijana ambaye alishiriki maandamano ya hapo awali.

    “Wahalifu wamefanya vitendo vya mabavu kwa kuiba, kupora na kuharibu mali,” amesema Kimeu, akibainisha kuwa waandamanaji waliingia mitaani kudai mageuzi kutoka kwa serikali, ikiwa ni pamoja na kufutwa kazi kwa maafisa wanaotuhumiwa kwa ufisadi. Waandamanaji pia waliitaka serikali kuomba radhi na kutoa fidia kwa familia za waliouawa wakati wa makabiliano na polisi na vikosi vya usalama.

    "Timu zetu za uchunguzi wa jinai zimetumwa kuwakamata wahalifu waliorekodiwa na kuhusika na kuibia Wakenya wasio na hatia barabarani huku wakichukua fursa ya maandamano yanayoendelea," Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai ya Kenya imesema katika taarifa. "Yeyote anayehusika na vitendo vya uhalifu anakumbushwa kuwa sheria itawakamata." Imeongeza

    Rais Ruto kuondoa bungeni hatua za ushuru zilizoainishwa katika Mswada wa Fedha wa Mwaka 2024, ambao ulilenga kuongeza shilingi bilioni 346.7 (karibu dola bilioni 2.7 za Kimarekani) kufadhili bajeti ya dola bilioni 31 kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025, hakukufaulu kuzima machafuko hayo ya umma. Licha ya wito wake wa mazungumzo, maandamano yamebadilika kuwa ya vurugu, na kuongeza mvutano wa kisiasa na kuvuruga biashara ya kawaida katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki.

    Kamati ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) iliripoti Jumatatu kwamba watu takriban 39 walikuwa wameshafariki katika maandamano hayo yaliyofanyika sehemu mbalimbali nchini , idadi ambayo imeongezeka hadi 41 kufikia Jumanne, huku wengine 361 wakiwa wamejeruhiwa.

    Viongozi kadhaa wa kimataifa wamehimiza kujizuia ili kuzuia kupamba moto kwa msukosuko huo wa kisiasa. Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa wito kwa wadau wahusika wa maslahi ya kitaifa kushiriki katika mazungumzo ya kiujenzi na kushughulikia masuala yenye utata.?

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha