<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Kundi la Watafiti washuhudia idadi kubwa ya nyangumi na pomboo kwenye eneo la bahari la Mashariki la Kisiwa cha Hainan, China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024
    Kundi la Watafiti washuhudia idadi kubwa ya nyangumi na pomboo kwenye eneo la bahari la Mashariki la Kisiwa cha Hainan, China
    Picha iliyopigwa tarehe 5, Julai ikionesha kundi la nyangumi wenye mapezi mafupi wakiogelea kwenye eneo la bahari la Mashariki la Kisiwa cha Hainan, China.

    Hivi karibuni, kundi la watafiti wa “wanaofuatilia nyangumi ‘Haitang’ na Bionuwai ya Baharini" wameshuhudia idadi kubwa ya nyangumi na pomboo kwenye eneo la bahari la Mashariki la Kisiwa cha Hainan, China, wakiwemo nyangumi wa jamii ya kujiongoza katika makundi wenye mapezi mafupi na pomboo aina ya Fraser.

    Watafiti hao wameeleza kuwa, kundi la nyangumi na pomboo hao waliowashuhudia mara hii linajumuisha jozi nyingi za mama na mtoto, hali ambayo inaonesha bioanuwai tajiri ya Bahari ya Kusini mwa China.

    Shughuli hiyo ya utafiti imefanywa kwa pamoja na Idara ya Bahari ya Hainan, Idara ya Mambo ya Kilimo na Vijiji ya Sanya, Taasisi ya Sayansi na Uhandisi wa Bahari ya Kina ya Akademia ya Sayansi ya China, na Jumuiya ya Ulinzi wa Bahari ya Utepe wa Bluu.

    (Picha na Zhang Liyun/Xinhua)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha