<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    “Treni za miambani za masafa mafupi”?zatoa uzoefu usio na kifani wa usafiri wa kitalii mashariki mwa China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2024
    “Treni za miambani za masafa mafupi”?zatoa uzoefu usio na kifani wa usafiri wa kitalii mashariki mwa China
    “Treni ya miambani ya masafa mafupi” ikiendeshwa kwenye kivutio cha watalii cha Mlima Dajue katika Mkoa wa Jiangxi, China, Julai 10, 2024.

    Treni za utalii wa kutazama mandhari zinazoendeshwa kwenye miamba ya eneo la milima mirefu kwa kutumia reli moja na mfumo wa njia zilizoundwa na Kampuni ya Teknolojia ya Vifaa Maalum ya Zhuzhou CRRC zimekamilika na kupelekwa kwenye kivutio cha watalii cha Mlima Dajue katika Mkoa wa Jiangxi wa China, siku ya Jumatano, Julai 10.

    Njia nzima ya reli ya mradi huo wa “treni ya miambani ya masafa mafupi” imepachikwa kwenye pande za mlima, na zaidi ya theluthi moja ya njia hiyo iko karibu ya miamba, ikiwafanya watalii kuwa kwenye mwinuko wa mita 850 hadi 1,150, pamoja na sifa ya “kuvutia, hatari, ajabu” na nyinginezo. Mhusika wa mradi amesema kuwa mradi huo unatumia muundo wa treni ya mabehewa sita yenye uwezo wa kubeba abiria 56.

    (Mpiga picha: Guo Wenjie/Xinhua)

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha