<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mwonekano wa usiku wa eneo la kivutio cha utalii cha Lango la Jiayu katika Mkoa wa Gansu, China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2024
    Mwonekano wa usiku wa eneo la kivutio cha utalii cha Lango la Jiayu katika Mkoa wa Gansu, China
    Picha hii iliyopigwa Julai 14, 2024 ikionyesha ukuta wa mji wa kale ukiwa unang’aa kwa taa wakati wa usiku kwenye eneo la kivutio cha utalii cha Lango la Jiayu katika Mji wa Jiayuguan, Mkoa wa Gansu, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Ma Ning)

    Lango la Jiayu katika Mji wa Jiayuguan, Mkoa wa Gansu, Kaskazini-Magharibi mwa China ni mahali pa kuanzia kwa sehemu ya Ukuta Mkuu wa China uliojengwa wakati wa Enzi ya Ming (1368-1644). Lango hilo pia lilitumika kama sehemu muhimu ya kupitia kwenye Njia ya Kale ya Hariri.

    Kuanzia tarehe 15 Julai, Lango hilo maarufu la Jiayu litafunguliwa rasmi kwa ajili ya utalii wa usiku, likionesha maudhui yanayohusu utamaduni wa Ukuta Mkuu wa China na Njia ya Hariri. Ukitumia mchanganyiko wa projekta za leza, teknolojia ya kidijitali, na maonyesho ya moja kwa moja jukwaani, utalii huo wa usiku unalenga kuwapa watalii uzoefu na uchangamani wa kipekee wa mwanga.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha