<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Maonyesho makubwa kuhusu ustaarabu wa kale wa Misri yafunguliwa Shanghai (8)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2024
    Maonyesho makubwa kuhusu ustaarabu wa kale wa Misri yafunguliwa Shanghai
    Picha hii iliyopigwa Julai 17, 2024 ikionyesha kichwa kutoka kwenye sanamu Nefertiti kwenye maonesho kabla ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho ya "Kilele cha Piramidi: Ustaarabu wa Misri ya Kale" kwenye Jumba la Makumbusho la Shanghai nchini China. (Xinhua/Liu Ying)

    SHANGHAI - Maonyesho makubwa ya ustaarabu wa kale wa Misri, ambayo ni makubwa zaidi ya aina yake kufanyika nje ya Misri katika miaka 20 iliyopita, yamefunguliwa siku ya Jumatano mjini Shanghai, mashariki mwa China ambapo mabaki ya kale jumla ya 788 kutoka Misri, pamoja na mabaki ya kale ya China, yanaonyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Shanghai, yakiwapa watembeleaji wake uhondo wa sanaa kutoka kwenye ustaarabu huo wa kale.

    Maonyesho hayo, "Kilele cha Piramidi: Ustaarabu wa Misri ya Kale" yameandaliwa kwa pamoja na Jumba la Makumbusho la Shanghai na Halmashauri Kuu ya Mambo ya Kale ya Misri (SCA).

    Kazi za kupangia, kuchagua na kuandaa maaonesho zilifanywa na wasomi wa China. Maonyesho hayo yameonesha ustaarabu wa Misri ya kale wa pande zote, na yanaonyesha matokeo mapya ya ushirikiano kati ya China na Misri katika kazi ya utafiti wa mabaki ya kale.

    Luo Wenli, naibu mkuu wa Idara ya Kitaifa ya Mabaki ya kale ya Kitamaduni ya China, amesifu maonyesho hayo ni daraja la mazungumzo kati ya China na Misri, ambazo zote ni nchi za ustaarabu wa kale.

    Miongoni mwa vitu vinavyooneshwa ni sanamu za Miungu waliosimuliwa kwenye hekaya na falsafa ya Misri ya kale, vyungu vya rangi vilivyofinyangwa kabla ya historia na vibao vya vipodozi, pamoja na hazina kutoka enzi tofauti za utawala wa China ya kale na fharao mbalimbali za Misri.

    Kwenye ukumbi wa pili wa maonyesho, vitu zaidi ya 400 vipya vilivyofukuliwa kutoka Saqqara, eneo muhimu la makaburi katika Misri ya kale, ambavyo vinaonyeshwa kwa mara ya kwanza duniani. Ukumbi huo pia unaonyesha mafanikio makubwa ya ushirikiano kati ya China na Misri katika kazi ya utafiti wa mambo yale katika kipindi cha karibuni.

    Xue Jiang, kiongozi wa mradi na msomi wa taaluma za Misri ya kale kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Shanghai amesema katika siku zijazo, maktaba ya data za utafiti wa pamoja wa kiakiolojia kati ya China na Misri yataanzishwa ili watu wa duniani watanufaika pamoja na matokeo ya utafiti, na utambuzi wa matokeo hayo utatolewa kwa Dunia nzima kwa lugha za Kichina, Kiingereza na Kiarabu.

    Mohamed Ismail Khaled, Katibu Mkuu wa SCA ya Misri, amesema kuwa maonyesho hayo yanaonyesha fahari ya ustaarabu wa kale wa Misri na uanuai wa jamii ya Misri.

    Ameelezea matumaini kwamba vitu hivyo vyote vinavyooneshwa vinaweza kuwa mabalozi wa kitamaduni wa Misri. Pia amewaalika watu wa China kutembelea Misri na kujionea ustaarabu wake mzuri.?

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha