<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Habari picha: Maisha ya mwalimu kujitolea kwenye elimu katika?Kijiji cha Shenyang, China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2024
    Habari picha: Maisha ya mwalimu kujitolea kwenye elimu katika?Kijiji cha Shenyang, China
    Ma Rusong akionyesha rula ya pembetatu ambayo amekuwa akiitumia katika maisha yake yote ya kufundisha nyumbani katika Kijiji cha Shenyang cha Mji wa Taizhou, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Julai 30, 2024. (Xinhua/Li Bo)

    Ma Rusong mwenye umri wa miaka 84, aliwahi kuwa mwalimu katika shule ya sekondari ya Dalun iliyoko Taizhou, Mkoa wa Jiangsu, nchini China. Alirudi katika Kijiji cha Shenyang alikozaliwa Mwaka 2001. Kutokana na kuwepo kwa watoto wengi walioachwa kijijini hapo na wazazi ambao ama wamefariki au kwenda mijini kufanya kazi, aliamua kutoa masomo bila malipo kwa watoto hao katika nyumbani kwake.

    Alitoa masomo ya hisabati, fizikia na kemia siku za wikendi na likizo za shule, na pia kutilia maanani afya ya akili ya watoto. Maelfu ya wanafunzi wamenufaika kutokana na hatua nzuri hizo za Ma katika miongo miwili iliyopita.

    Ma amesema yeye mwenyewe aliwahi kuwa yatima, na asingeweza kuwa mwalimu bila uungaji mkono wa kijamii. Anataka kulipa wema huo aliopata wakati wowote huduma yake inapohitajika.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha