<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mji wa Zhuji wa China yaendeleza sekta ya matunda maalum ili kuwezesha ustawi wa vijiji (3)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2024
    Mji wa Zhuji wa China yaendeleza sekta ya matunda maalum ili kuwezesha ustawi wa vijiji
    Picha iliyopigwa Agosti 7 ikionyesha Kijiji cha Huangjiadian cha Huangshan, China. (Xinhua/Xu Yu)

    Kwa sasa ni msimu wa kuchuma pichi. Kijiji cha Huangjiadian cha Huangshan, Mji wa Zhuji, Mkoa wa Zhejiang, China kimeingia katika msimu mzuri wa mavuno, na matunda ya pichi yanaonekana yakining’inia kwenye matawi. Katika wakati huu, kuna mu karibia 1,000 (takriban hekta 66.67) za mashamba ya pichi katika Kijiji cha Huangjiadian, na kuna familia 10 kubwa zenye eneo la kupanda pichi lenye ukubwa wa zaidi ya mu 50 (hekta 3.33 hivi). Mwaka huu, mapato ya kijiji hicho kutokana na pichi ni karibu yuan milioni 3.

    Katika miaka ya hivi karibuni, mji mdogo wa Huangshan wa Mji wa Zhuji umehimiza maendeleo ya sekta ya matunda maalum na utalii wa vijijini, ikianzisha ushirika wa matunda, na matangazo ya moja kwa moja ya mauzo mtandaoni, kustawisha sekta ya utalii wa kilimo na kujenga maeneo mazuri ya utalii wa kilimo ili kuwezesha watu kuongeza mapato na kustawisha vijiji.?

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha