<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mfanyakazi Kijana wa kutunza nyaya za umeme unaotumiwa na treni za reli alinda safari za majira ya joto

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2024
    Mfanyakazi Kijana wa kutunza nyaya za umeme unaotumiwa na treni za reli alinda safari za majira ya joto
    Chen Chuyan akikagua waya wa umeme wa kutumiwa na treni za mwendokasi juu ya reli ya Yulin-Tieshangang, China, tarehe 7, Agosti.

    Akiwa alizaliwa Mwaka 2000, Chen Chuyan ni mmoja kati ya wafanyakazi wanawake wachache wa kutunza nyaya za umeme unaotumiwa na treni za mwendokasi juu ya reli wa Kampuni ya Reli ya Guangxi Yanhai, Tawi la Qinzhou.

    Reli ya Yulin-Tieshangang ni sehemu muhimu ya Ukanda Mpya wa Biashara ya Nchi Kavu na Baharini wa Magharibi mwa China, na pia ni sehemu ambayo Chen na wenzake wanabeba jukumu la kutunza na kukarabati nyaya zake za umeme.

    Chen mara zote huwa anawahi mstari wa mbele na kufanya kazi ya kukagua na kukarabati nyaya za umeme juu ya reli kwa umakini. Amesema, "Wanawake si duni kwa wanaume. Ni kawaida kufanya kazi ngumu na kuvuja jasho. Sasa ni muda wetu, vijana wa 'kizazi cha kuzaliwa baada ya 2000', kuonyesha kuwajibika kwetu kuhakikisha usalama wa reli.”

    Picha na Zhang Ailin/Xinhua

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha