Lugha Nyingine
Katika picha: Walinzi wa miti iliyo hatarini kutoweka katika Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China
Miti mwitu ya Thuja sutchuenensis ni mimea maalum ya gymnosperm iliyo ya hatarini kutoweka nchini China, na imepata uhifadhi wa ngazi ya kwanza. Mwaka 1998, Shirikisho la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira lilitangaza kuwa Thuja sutchuenensis imetoweka, lakini mimea hiyo iligunduliwa tena katika Wilaya ya Chengkou mwaka 1999. Kwa sasa, idadi ya mimea mizima ya Thuja sutchuenensis duniani ni chini ya 10,000, na inatapakaa tu katika maeneo ya milima ya Eneo la Kaizhou na Wilaya ya Chengkou zilizoko sehemu za Mlima Daba za mji wa Chongqing.
Ili kuhifadhi aina hiyo ya mimea iliyo ya hatarini kutoweka, Yang Quan kutoka Hifadhi ya kitaifa ya Xuebaoshan ya Chongqing aliongoza timu kufanya uchunguzi na utafiti wa jumuiya ya miti mwituni ya Thuja sutchuenensis, akitumaini kupanua jumuiya ya miti hiyo.
Kwa kupitia juhudi za miaka mingi, timu ya utafiti ilichagua kuchukua vipandikizi kama njia ya kutimiza ukuaji wa miti mwituni ya Thuja sutchuenensis kwenye maeneo makubwa. Hadi sasa, jumla ya mimea hiyo milioni 2.7 imeoteshwa na kukua kwa njia ya kibinadamu.
Kuanzia Mwezi Machi,Mwaka jana, mimea ya Thuja sutchuenensis imepandwa pia kwenye vituo18 vya majaribio vilivyoko katika mikoa 11 pamoja na mikoa inayojiendesha, kama vile Mikoa ya Yunnan, Ningxia, Shaanxi, Gansu na Xizang kwa ajili ya uhifadhi wa uhamiaji na upandaji wa kuzoea hali ya sehemu tofauti.
“Tunatumai kuchukua Thuja sutchuenensis kama mfano wa kuigwa, na kupanua uzoefu wetu katika kazi za uokoaji na ulinzi wa mimea iliyo ya hatarini kutoweka ," Yang Quan alisema.(Xinhua/Huang Wei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma