Lugha Nyingine
Idadi ya tumbili wenye manyoya ya dhahabu yaongezeka katika Eneo la Misitu la Shennongjia nchini China (3)
Eneo la Misitu la Shennongjia katika Mkoa wa Hubei, katikati ya China limeripoti kuwa, idadi ya tumbili wenye manyoya ya dhahabu inaongezeka siku hadi siku kutokana na juhudi za kulinda makazi ya tumbili hao.
Matokeo ya uchunguzi wa 4 uliofanywa na serikali ya eneo hilo yameonesha kuwa, hivi sasa eneo hilo limekuwa na tumbili wenye maonyoya ya dhahabu 1,618, ambao wameongezwa 147 kuliko waliohesabiwa katika uchunguzi uliofanywa katika miaka mitano iliyopita.
Ikiwa linajulikana kwa muda mrefu kwa uzuri wake wa mazingira ya asili na bioanuwai nyingi, katika miaka mingi iliyopita, Eneo la Misitu la Shennongjia limeendelea kuboresha bioanuwai na utulivu wa mfumo wake wa ikolojia siku hadi siku, na kuhimiza kwa pande zote usimamizi wa mifumo ya milima, mito, misitu, mashamba, maziwa na mbuga. Ubora wa mazingira ya ikolojia katika eneo hilo umeendelea kuimarika, huku ueneaji wa misitu ukidumishwa kwa asilimia 91.12.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma