Lugha Nyingine
Mhifadhi Mazingira wa China Atoa mchango?katika?Uhifadhi wa Wanyama?Pori Nchini Kenya
Zhuo Qiang akikagua hali ya ng'ombe aliyeshambuliwa na simba katika familia ya Wamaasai huko Maasai Mara, Kenya, Agosti 22, 2024. (Xinhua/Wang Guansen) |
Kuanzia kutazama katuni zinazoonyesha wanyama pori utotoni hadi kuwa mhifadhi wa Wanyama pori, Zhuo Qiang, aliyepewa jina la utani Simba, ni Mchina wa kwanza anayefanya kazi ya uhifadhi wa wanyama pori barani Afrika.
Mwaka 2011, Zhuo Qiang alikwenda mbuga ya Maasai Mara-Serengeti, ambapo alikuwa akiishi na Wamaasai na kufanya kazi na wahifadhi wenyeji katika Hifadhi ya Wanyama Pori ya Ol Kinyei. Ameendelea kufanya kazi zake huko mpaka sasa.
Kazi yake ni pamoja na kushika doria katika hifadhi ili kuzuia ujangili wa wanyama pori na malisho haramu, kufuatilia wanyama pori na kuokoa wanyama wanaojeruhiwa.
Zhuo Qiang anaamini kwamba uhifadhi wa wanyama pori unahitaji kushirikishwa na jamii za kienyeji. "Uhifadhi wa wanyama pori unawezekana tu kama watu wakishikamana." alisema.
Hali kadhalika, utalii wa unaozingatia uhifadhi wa mazingira umechukuliwa kuwa chaguo zuri la kuendeleza uchumi wa eneo hilo na kusaidia Wamaasai kuishi maisha mazuri zaidi bila kuua wanyama, Zhuo Qiang alisema.
Kupitia juhudi za miaka mingi, Zhuo Qiang amepata uaminifu na heshima kutoka kwa makabila ya kienyeji.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma