<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mrithi wa Wimbo?wa Kabila la Wadong

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2024
    Mrithi wa Wimbo?wa Kabila la Wadong
    Agosti 28, wenyeji na watalii wakinywa pombe kwenye karamu katika Kijiji cha Chengyangbacun cha Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wadong ya Sanjiang ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, China. (Xinhua/Zhang Ailin)

    Wilaya ya Kabila la Wadong ya Sanjiang ya Mkoa wa Guangxi ambayo ina wakazi wengi zaidi wa Kabila la Wadong nchini China, inajulikana kwa utamaduni wa aina mbalimbali wa Kabila la Wadong. Wimbo wa Kabila la Wadong imeorodheshwa kwenye orodha ya vitu vya urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa wa China mwaka 2009.

    Wu Chunyue mwenye umri wa miaka 37 ndiye mrithi wa Wimbo wa Kabila la Wadong, amejitolea katika uvumbuzi wa kwaya za Kabila la Wadong, akichanganya ala za kijadi na vipengee vya muziki vya kisasa ili kuvumbua mtindo mpya wa kuonyesha. Zaidi ya hayo, Wu Chunyue amekuwa akiendelea kufanya kazi za shambani, kuwasiliana na wanavijiji na watalii wa eneo hilo ili kupata wazo kutoka maisha. Juhudi zake zimevutia vijana wengi zaidi kufuatilia utamaduni wa Kabila la Wadong.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha