Lugha Nyingine
China yashuhudia kuongezeka kwa safari za kitalii wakati wa likizo ya Sikukuu ya Jadi ya Mbalamwezi (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2024
Watu wakitembelea kivutio cha watalii cha Mapango ya Longmen katika Mji wa Luoyang, Mkoa wa Henan, Katikati mwa China, Septemba 16, 2024. (Picha na Li Weichao/Xinhua) |
BEIJING - Safari za abiria takriban milioni 629.56 zimeshughulikiwa na sekta za usafirishaji nchini China wakati wa likizo ya siku tatu ya Sikukuu ya Jadi ya Mbalamwezi ya China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.1 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, takwimu kutoka Wizara ya Uchukuzi ya China zimeonyesha siku ya Jumatano.
Kwa jumla, China imerekodi safari za abiria milioni 42.57 kwa njia ya reli, milioni 1.98 kwa maji, na milioni 5.07 kwa ndege.
Safari za kutumia magari barabarani zilichukua sehemu kubwa, huku zikiwa na safari milioni 579.94 za abiria.
Sikukuu ya Jadi ya Mbalamwezi ya China iliangukia Septemba 17 mwaka huu.?
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma