<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Hezbollah yathibitisha kiongozi wake Nasrallah kuuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel mjini Beirut (5)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2024
    Hezbollah yathibitisha kiongozi wake Nasrallah kuuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel mjini Beirut
    Picha hii iliyopigwa Septemba 28, 2024 ikionyesha majengo yaliyobomolewa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel katika kitongoji kusini mwa Beirut, Lebanon, Lebanon. (Xinhua/Bilal Jawich)

    BEIRUT/GAZA - Hezbollah imethibitisha Jumamosi kwamba kiongozi wake Sayyed Hassan Nasrallah ameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga makao makuu ya kamandi ya kundi hilo siku moja mapema huko Dahieh, kusini mwa Beirut ambapo katika taarifa yake, kundi hilo limemuomboleza Nasrallah, likimuelezea kuwa "mhanga mkubwa" na "kiongozi shujaa, shupavu, jasiri, mwenye busara, mwerevu na mwaminifu" kwa karibu miaka 30, ambaye hivi karibuni aliongoza katika "vita vya Palestina, Gaza na watu wanaokandamizwa wa Palestina."

    Muda mfupi baada ya Hezbollah kuthibitisha kifo cha Nasrallah, Hamas ilitoa taarifa ikitoa "rambirambi zake za dhati, pole, na mshikamano kwa ndugu wa Lebanon" na "ndugu zake katika Hezbollah na Vuguvugu la Kiislamu nchini Lebanon."

    Pia imelaani mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Dahieh kuwa ni "kitendo cha kigaidi cha woga, mauaji ya halaiki na uhalifu mbaya wa kijinai" ambayo inathibitisha kwa mara nyingine "umwagaji damu na ukatili wa Israel."

    Hamas imeitaja Israel kuhusika kikamilifu kwa "uhalifu huu mbaya na madhara yake makubwa kwa usalama na utulivu wa eneo hilo," na kulaani "uungaji mkono unaoendelea" wa utawala wa Marekani kwa Israeli.

    Ijumaa jioni, ndege za kivita za Israel zilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya makao makuu ya Hezbollah huko Dahieh, ambayo kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Ulinzi la Israel mapema Jumamosi, yamemuua Nasrallah na baadhi ya makamanda wengine wa kundi hilo lenye silaha.

    Mashambulizi hayo yameporomosha majengo kadhaa ya makazi, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua sita, majeruhi 91, na uharibifu mkubwa wa miundombinu katika eneo hilo, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha MTV cha Lebanon.

    Israel imekuwa ikizidisha mashambulizi yake ya anga kote Lebanon tangu Jumatatu, ikiwa ni hatua kubwa zaidi ya kijeshi ya Israel kuwahi kutokea nchini humo tangu Mwaka 2006.

    Hii inaashiria kuongezeka kwa mapigano yanayoendelea yaliyoanza Oktoba 8, 2023, wakati Hezbollah ilipoanza kurusha roketi huko Israel katika kuonesha mshikamano na Hamas katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha Israel kufanya mashambulizi ya kulipiza ya makombora na ya anga kusini mashariki mwa Lebanon.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha