Lugha Nyingine
Sekta ya nishati mpya ya China yanufaisha mageuzi ya kijani ya Malaysia (5)
Noor Azie Syamira, mfanyakazi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua akionekana pichani mjini Kuala Ketil, Malaysia, tarehe 6 Juni, 2024. (Picha na Chong Voon Chung/Xinhua) |
KUALA LUMPUR - Huko Kuala Ketil, sehemu ya kusini ya Jimbo la Kedah la Malaysia, kuna kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua ambacho kina eneo lenye ukubwa wa ekari 260. Kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawati 50 kilijengwa na kampuni ya ujenzi wa nishati ya umeme ya Tianjin chini ya kundi la kampuni za uhandisi wa nishati la China (China Energy Engineering Group Tianjin Electric Power Construction) kilianza kufanya kazi Mwaka 2019.
Kwa kuendana na mwelekeo wa kimataifa wa kuondoa hewa ya kaboni na maendeleo endelevu, Malaysia imekuwa ikifanya kazi kwa bidii katika miaka ya hivi karibuni ili kuondokana na utegemezi wake kwa nishati ya mafuta kupita kiasi na kuongeza matumizi ya nishati mbadala katika uzalishaji wake wa nishati. Hadhi ya China ya kuongoza katika sekta ya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua siyo tu inatoa vifaa lakini pia inatoa teknolojia kwa mageuzi ya kijani ya Malaysia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma