Lugha Nyingine
Peng Liyuan pamoja na wake wa viongozi wa Afrika wahudhuria mkutano kuhusu elimu ya wanawake (5)
Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni balozi maalum wa kuhimiza elimu ya watoto wa kike na wanawake wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), pamoja na wageni wa Afrika, wakitembelea vitu vya maonyesho vinavyoonyesha utamaduni wa jadi na mafanikio ya China katika elimu ya wanawake kwenye Mkutano wa Mada Mahsusi kuhusu Elimu ya Wanawake wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024 (Xinhua/Xie Huanchi) |
BEIJING - Peng Liyuan, mke wa Rais wa China Xi Jinping, amehudhuria mkutano kuhusu elimu ya wanawake wa China na Afrika siku ya Alhamisi na kutoa hotuba, ambapo wake wa viongozi wa Afrika wapatao zaidi ya 20, ambao wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), wameshiriki kwa pamoja katika shughuli za mkutano huo.
Katika hotuba yake, Peng amesema China na Afrika ni za jumuiya yenye mustakabali wa pamoja na kwamba wanawake wa China na Afrika kwa bidii, hekima na kujitolea, wameandika ukurasa usio na kifani wa mshikamano, ushirikiano na maendeleo.
Katika kuendeleza elimu ya wanawake na kuelekea katika mustakabali mzuri zaidi, China na Afrika zinaendana katika malengo yao, Peng ameeleza.
Kwenye mkutano huo, Marie Khone Faye, mke wa Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, na washiriki wengine wa mkutano pia walitoa hotuba.
Wamemshukuru Peng kwa mchango wake bora katika kuhimiza elimu ya watoto wa kike na wanawake wa Afrika na kusifu uungaji mkono na msaada wa muda mrefu wa China katika nyanja husika.
Peng na wageni wa Afrika pia walifurahia uimbaji wa watoto na Opera ya Beijing na vitu vya maonyesho vinavyoonyesha utamaduni wa jadi wa China na mafanikio katika elimu ya wanawake.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma